09/09/2026
Waziri wa Madini wa Kenya, Ali Hassan Joho, akiongozana na Mbunge wa Kapsaret, Oscar Sudi, wamewasilisha salam zao za rambirambi na kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba mzito wa kuondokewa na mumewe mpendwa, Hafidh Ameir.
Viongozi hao wameeleza kuwa Kenya inasimama pamoja na Rais Samia, familia yake, na wananchi wote wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu cha simanzi na maombolezo.
"Tunamwombea Mwenyezi Mungu ampe Mheshimiwa Rais na familia yake subira, amani, na afueni ya moyo wakati huu wa majonzi makuu. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un." — Ali Hassan Joho.
Rambirambi