Fredy Njeje Photography

Fredy Njeje Photography I Do Photography This is my official Blog where i post different types of News

Katika siku ya leo ya Kupiga picha Duniani  nikiwa mpiga picha Mzawa wa Tanzania nikijikita katika picha za utalii na ku...
19/08/2026

Katika siku ya leo ya Kupiga picha Duniani nikiwa mpiga picha Mzawa wa Tanzania nikijikita katika picha za utalii na kuonesha uzuri waTanzania na kwa hamasa hii namshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Tanzania kwa kuwa Muongoza njia na Kinara katika Masuala ya Utalii Tanzania kwa hakika ameiweka Tanzania juu na kupitia Filamu ya Royal Tour nimehamasika zaidi kufikisha ujumbe kupitia upigaji picha , vile vile nawashukuru sana wadau wa Utalii Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿 Tanzania Unforgettable Tanzania Tourist Board Ngorongoro Conservation Area Tanapa Updates (TANAPA) Tanzania National Parks TAWA TANZANIA Tanzania Forest ServicesAgency Sam Nsyuka Paulina Mk**a Dos S Santos Msemaji Mkuu wa Serikali kwa uchache Taasisi hizi na wadau hawa wamekuwa wakinipatia ushirikiano mkubwa hasa nikiwa katika shughuli zangu za kupiga picha kutalii ikiwa ni kwa lengo la kuonesha uzuri wa Tanzania na Kuhamasisha watanzania waendelee kutembelea vivutio vyetu kupitia Kampeni yangu ya Hashtag . Mwisho usiache kutembelea ukurasa huu kila wakati.

Katika siku hii ya kupiga picha hata sisi wapiga picha huwa tunapigwa picha
19/08/2026

Katika siku hii ya kupiga picha hata sisi wapiga picha huwa tunapigwa picha

Leo Tarehe 19 Agosti 2026 ni siku ya kupiga picha Duniani ninajivunia kuwa Mpiga picha kutoka Tanzania na ninayetumia Ka...
19/08/2026

Leo Tarehe 19 Agosti 2026 ni siku ya kupiga picha Duniani ninajivunia kuwa Mpiga picha kutoka Tanzania na ninayetumia Kamera yangu kuonesha uzuri wa Nchi yangu na kutangaza vivutio vya nchi yangu kwa kituo. Picha ni sanaa hivyo naamini uzuri wa Tanzania upo katika kamera na macho yangu hapa ni nyumbani na ambapo kazi yangu ni moja tu kuhamasisha wazawa yaani watanzania kutembelea vivutio vyetu, ni sehemu yako nzuri ya kujionea mengi

Asante Tanzania

Samia Suluhu Hassan Tanzania Tourist Board Tanzania Unforgettable Ngorongoro Conservation Area

Katika moja ya maeneo ambayo nilipenda sana baada ya kutembelea na kupiga picha ni katika Hifadhi ya wanyamapori Pande J...
04/08/2026

Katika moja ya maeneo ambayo nilipenda sana baada ya kutembelea na kupiga picha ni katika Hifadhi ya wanyamapori Pande Jijini Dar es Salaam, wanyama unawaona vizuri sana. Hapa nimekuletea Twiga na Swala wanapatikana hapo, Swala utawaona weengi sana na utapata kujua Jike au Dume nani ana pembe pia utaelezwa kwa nini Swala dume hutengwa na mengine kibaoo.

Karibu utembelee eneo hili utaona unataka kuendelea kufurahia wanyama lakini muda utakuwa hautoshi hivyo utatakiwa kwenda na kwenda tena.

Cc: Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿 TAWA TANZANIA

Katika hifadhi ya wanyamapori Pande Jijini Dar es Salaam, kuna nyumbu ambao sifa yao kubwa sio wazurulaji yaani ni jamii...
04/08/2026

Katika hifadhi ya wanyamapori Pande Jijini Dar es Salaam, kuna nyumbu ambao sifa yao kubwa sio wazurulaji yaani ni jamii ya wasiohama hama k**a wale wengine utawakuta ukienda tembelea huko, usiishie kuwaona hawa nao wapiga hapa bali nenda kawashuhudie, pia kuna hao Pundamilia nao wapo kibao wanatembea tembea katika hifadhi hiyo.

Kikubwa usipange kukosa kutembelea huko utakuja kunishukuru



Cc: Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿 TAWA TANZANIA

Karibu Hifadhi ya Wanyamapori Pande hapa Simba huyu atakufurahisha mpaka ushangae hutakiwi kukosa kutembelea hapa.Cc: Uk...
04/08/2026

Karibu Hifadhi ya Wanyamapori Pande hapa Simba huyu atakufurahisha mpaka ushangae hutakiwi kukosa kutembelea hapa.

Cc: Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿 TAWA TANZANIA

Wengi mtakuwa na Hamu ya kufahamu Gharama za kuingia katika eneo hili bora kabisa, mimi nimesha waeleza mambo kibao ila ...
03/08/2026

Wengi mtakuwa na Hamu ya kufahamu Gharama za kuingia katika eneo hili bora kabisa, mimi nimesha waeleza mambo kibao ila sasa haya ya kiutendaji kujua ukitaka kujua kiingilio kwa watu wazima watoto na wale watoto kabisa mtaelezwa, mkitaka kufahamu gharama za kuingia na magari binafsi au ya tour na Mkitaka kufahamu gharama za Misosi(nyama pori choma, makange, kukaanga, ugali, ndizi, chips na vyakula vingine kibao) ikiwa ni pamoja na vivywaji kibao. Wasiliana moja kwa moja kwa instagram Pande Game Reserve pia tembelea akaunti yao TAWA TANZANIA kuona mambo yao mengine zaidi

Suala langu ni moja tuu kukusogezea maeneo ya utalii ili na wewe ukatembelee sasa eneo hili umesha liona, na picha ndio k**a hizo nilizopiga japo kwa uchache lakini umepata picha kubwa usikose kuwa hapo utakuja kunishukuru.

Cc: Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿 TAWA Central Zone Office Tanzania Unforgettable

Kuna aina mbalimbali za utalii ukiwa katika pori la hifadhi ya wanyamapori pande, unaweza kutumia Gari la utalii au  gar...
03/08/2026

Kuna aina mbalimbali za utalii ukiwa katika pori la hifadhi ya wanyamapori pande, unaweza kutumia Gari la utalii au gari binafsi ambalo ukiwa getini utashauriwa k**a utumie au lah, pia unaweza ukafanya utalii wa kutembea kwa miguu ambapo sehemu zote hizo kutakuwa na muongozaji utalii ambaye atakuwa kwa ajili ya kuongoza pia kutoa maelezo mbalimbali kuhusiana na eneo hilo, wakati huo wa kutalii pia utapata nafasi ya utalii wa kupiga picha.

Baada ya kutembelea na kuona wanyama mpaka kuwakinai, baada ya hapo utapata nafasi ya kwenda eneo la kujimwaga ambapo hapo utapata burudani huku ukijichana na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyama pori.

Suala langu ni moja tuu kukusogezea maeneo ya utalii ili na wewe ukatembelee sasa eneo hili umesha liona, na picha ndio k**a hizo nilizopiga japo kwa uchache lakini umepata picha kubwa usikose kuwa hapo utakuja kunishukuru.

Karibu  Hifadhi ya Wanyamapori  Pande, ndiyo hifadhi ndogo zaidi ya wanyama Tanzania nzima, hifadhii hii inaukubwa wa Ki...
03/08/2026

Karibu Hifadhi ya Wanyamapori Pande, ndiyo hifadhi ndogo zaidi ya wanyama Tanzania nzima, hifadhii hii inaukubwa wa Kilometa za mraba 15.39 ambapo ipo upande wa wilaya ya Ubungo na Kinondoni Jijini Dar es Salaam na inafikika kirahisi sana.

Hifadhi hii ipo vizuri sana kwa kuwa ukianza kutembelea humo ndani hautojutia utakutana na wanyama kibaoo k**a Simba, swala,pundamilia, pofu, twiga, Nyumbu, Kasongo pamoja na Chatu Mkuubwa, Mamba, Mbuni na wanyama wengine wakiwa wanajivinjari hapa na pale, pia utaweza kuwapiga picha na kuwaona jirani kabisa.

Suala langu ni moja tuu kukusogezea maeneo ya utalii ili na wewe ukatembelee sasa eneo hili umesha liona, na picha ndio k**a hizo nilizopiga japo kwa uchache lakini umepata picha kubwa usikose kuwa hapo utakuja kunishukuru.

K**a ulikuwa haufahamu basi ngoja nikwambie kwa ufupi kuhusu eneo hili la Isimila. Awali jina la Isimila lilitokana na j...
02/08/2026

K**a ulikuwa haufahamu basi ngoja nikwambie kwa ufupi kuhusu eneo hili la Isimila.

Awali jina la Isimila lilitokana na jina Pepisimike wahehe wanajua kwa kuwa ni neno lao, lakini kwa faida ya wengi maana yake ni makazi ya kudumu.

Eneo hili lilitambulika kwa mara ya kwanza miaka ya mwanzoni mwa 1950 ambapo watafiti wa mambo ya kale waliona masalia ya zama za kale bondeni, watafiti hao ambao ni F. Clark Howell, Carl Hansen, Charles Caller, P. Bushozi, A. Mturi na wenzao walitumia muda wao kutafiti eneo hilo kwa kina ambapo pia walibaini kulikuwa na ziwa ambalo lilikuwa linavutia wanyama wengi kunywa maji na zamadamu alitumia eneo hilo kuwinda wanyama mbalimbali kwa ajili ya kitoweo.

Baada ya utafiti sana Serikali ya Kikoloni ya Uingereza ikaamua kutangaza eneo hilo kuwa ni hifadhi ya malikale mwaka 1958, na sasa eneo hilo lipo chini ya Serikali na likisimamiwa kwa karibu na Tanzania National Parks

Ili kupata mambo mazuri ya hapa k**a mimi nilivyofika hapo na kukusogezea picha na hamasa yangu kupiitia basi na wewe Mtanzania mwenzangu hakikisha unafika eneo hilo utanishukuru kwa kuwa huko ni zaidi ya Kuzuri, eneo lipo Iringa

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fredy Njeje Photography posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Fredy Njeje Photography:

Shortcuts

Share